ya juu ni VIDEO YAKE
Ram Singh
Mmoja kati ya washukiwa sita wa kesi ya
ubakaji huko India Bw. Ram Singh(33) amejinyonga hadi kufa akiwa
gerezani(Tihar mjini Delhi's Tihar) kwa kutumia nguo zake (blanket). Pia
alitumia ndoo iliyokua kwenye chumba hicho kupanda juu na kujinyonga.
Ram pamoja na wenzake walituhumiwa kwa kosa la kumbaka na kupelekea kufa
kwa msichana wa miaka 23 ambaye alikua mwanafunzi wa chuo kikuu ndani
ya bus ambalo lilikua likiendeshwa na Ram. Tukio hili lilitokea mwezi
Desemba mwaka jana.
Hata hivyo Baba mzazi wa Ram amepinga kuwa
Ram alijinyonga, "Kuna mtu amemuua" alisema Baba wa Ram. Aliongeza kuwa
mwanae alikua akibakwa na wenzake gerezani na pia kupewa vitisho toka
kwa walinzi. Hali hii inampelekea kuamini kuwa aliuawa. Alidai kuwa
alimtembelea mwanae gerezani siku nne zilizopita na hakuonesha dalili
yoyote ya kuutoa uhai wake yeye mwenyewe.
No comments:
Post a Comment