Thursday, May 30, 2013

Albert Mangwea Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko Mbamba Bay kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha ambaye naye yuko Mbamba Bay kuwa watu watakutanika Mbezi kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa. Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni jinsi gani mwili huo utafika hapa. Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha familia watatoa taarifa.

Albert Mangwea
Baba Mdogo wa Marehemu Mzee Mangweha ambaye yuko
 Mbamba Bay kikazi, amesema kuwa wamekubaliana na kaka yake 
mkubwa yaani baba mkubwa wa Ngwair, David Mangweha 
ambaye naye yuko Mbamba Bay kuwa watu watakutanika Mbezi
 kwa msiba na pia mapokezi yatafanyika hapa Dar es salaam
 Mbezi Beach. Ingawa bado kikao cha familia nzima hakijafanyika
 lakini baba huyo mdogo amesema wanaweza kulazimika kuzika 
Morogoro sehemu ambayo baba yake alizikwa.
 
Baba huyo mdogo alisema kuwa kesho ndo watarudi Dar es Salaam 
pamoja na kaka yake yaani baba mkubwa wa marehemu. Kuhusu
 mwili kuletwa hapa Tanzania kutoka Afrika Kusini baba mdogo 
amesema kuwa mpaka sasa hawajajua jinsi gani mwili huo utafika 
hapa lakini kuna ndugu zao ambao tayari washaanza kufanya 
taratibu za kuwasiliana na ubalozi wa Afrika Kusini ili kujua ni
 jinsi gani mwili huo utafika hapa.
 
Kama kutakuwa na mabadiliko yeyote watakapowasili kesho 
baba mdogo na baba mkubwa baada ya kikao cha
 familia watatoa taarifa.

No comments:

Post a Comment