Mabinti wa Saudia wakiwa |
Monday, January 07, 2013 7:47 PM Katika hali ambayo haikutarajiwa, Msichana mmoja wa nchini Saudi Arabia, mwenye umri wa miaka 15, mkazi wa Jazan kusini mwa nchi hiyo, ametoroka kwa mumewe na kurudi kwa wazazi wake, akipinga kuolewa na mzee. |
|
Msichana
huyo alipatwa na hofu kubwa kuolewa na babu huyo, na alipofika nyumbani
kwa mume wake alingia chumbani na kujifungia kwa muda wa siku mbili
mfululizo, na kisha kurudi nyumbani kwao, Bwana harusi amelichukulia
tukio hilo kama mbinu ya kumuibia pesa zake za mahari alizolipa. Mzee huyo ameliambia Gazeti la Al-Hayat la nchini Saudia, kuwa kesho (leo) Jumaatatu anatarajia kwenda Mkoani Hurata, kwa wazazi wa binti huyo ili kumchukua mke wake au apewe pesa zake za mahari alizotoa, Gazeti la Al-Hayat alikutaja umri wa bau huyo lakini lilimtaja kuwa ni mtu mzima sana. Kwa upande wake Mjumbe wa Bunge la Haki za Binadamu la nchi hiyo, Bi. Suhaila Zaini Abidin, ametoa wito kwa vyombo vinavyohusika kuingilia kati haraka suala hilo ili kumuoka mtoto huyo na janga hilo, Bi. Suhaila akiongea kwa masikitiko alisema, hakuna makubaliano kati ya wanandoa wenye utofauti mkubwa wa umri kati yao. Akibainisha kuwa moja ya masharti ya ndoa hayakufuatwa, kitendo cha mtoto huyo kujifungia mlango mwenyewe, hii inaonyesha wazi kuwa hakuna ridhaa ya ndoa, Suhaila aliwatupia lawama wazazi wa binti huyo kwa kusema, kuwa suala hili ni moja ya masuala kadhaa yanayotokea, ambayo yanasababishwa na wazazi kuwalazimisha mabinti zao kuolewa wakiwa na umri mdogo. |
Sunday, May 26, 2013
Binti Wa Miaka 15 Atoroka kwa Mume kisa Mzee
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment