Robert Schiavelli |
Friday, March 15, 2013 3:43 PM Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Schiavelli (42) amefikishwa kizimbani mjini new york kwa tuhuma za kuchafua hali ya amani na utulivu kwa kucheka kwa sauti kubwa. |
|
Mtu
mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Schiavelli (42) amefikishwa
kizimbani mjini new york kwa tuhuma za kuchafua hali ya amani na utulivu
kwa kucheka kwa sauti kubwa. Schiavelli ni mkazi wa kitongoji cha Rockville Center katika jimbo la New York nchini Marekani, alisema kamwe hakuwai kufikiria kwamba ipo siku kucheka kwa sauti ya juu kuna weza kumletea matatizo kiasi cha kufikishwa katika vyombo vya sheria. Schiavelli alikamatwa nyumbani kwake baada ya malalamiko ya majirani zake, Schiavell anasumbuliwa na ulemavu wa mishipa ya fahamu na amekuwa akitumia kucheka kwa sauti ya juu kama mbinu ya kujirinda. Polisi katika kituoa cha Rockville Center,imempiga faini Schiavelli ya dola 250 au kwenda jela siku 15, kwa kosa la kuvuruga amani wakati wa usiku. Wakili anayemtetea Schiavelli, bwana Andrew Campanelli amesema kuwa atapambana kwa nguvu zote kuhakikisha mteja wake anatoka jela. |
Sunday, May 26, 2013
Jela Au Faini Kwa Kucheka Kwa Sauti Kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment