Thursday, July 11, 2013

Mwanachuo ajilipua Saluni

MWANAFUNZI wa Chuo cha Ufundi (VETA) Dodoma, Taliki Juma, (22) amefariki baada ya kujilipua kwa mafuta ya petroli na kupelekea kujeruhiwa kwa wengine wenzake nane waliokuwa eneo hilo.

Mwanafunzi huyo alijiondoa uhai wake juzi majira ya jioni ya saa 10 huko eneo la Nzuguni nje kidogo ya mji wa Dodoma akiwa saluni.

Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Suzan Kaganda, saluni hiyo ilitambulika kwa jina la Tonny Hair Dressing Saloon inayomilikiwa na Irene.

Kaganda amesema, mwanafunzi huyo alinunua petrol kiasi cha lita tano na alipokwenda saloni hapo alijimwagia na kujiwasha hali iliyosabbisha waliokuwemo ndani ya saluni hiyo kujeruhiwa vibaya

Amesema kabla ya tukio hilo wenzake walimsihi asifanye kitendo hicho na hakuweza kuwaelewa na kuamua kufanya kitendo hicho cha kinyama akiwa katika saluni hiyo

Hata hivyo taarifa hiyo imesema, uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa, chanzo cha tukio hilo linahusiana na mambo ya kimapenzi licha ya Polisi kuendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo.

Mwanafunzi huyo imedaiwa kuwa alikuwa akisomea fani ya ufundi magari kutoka chuoni hapo

Majeruhi wote walilazwa katika hospitali ya mkoa wa Dodoma wakiwemo wanafunzi wawili mmmoja akiwa ni wa darasa la nne na mwingine akiwa ni mwanafuzi wa kidato cha pili na wengine ni wafanya biashara na waliokuja kupata huduma karibu na saluni hiyo

No comments:

Post a Comment