THE WORST VALENTINE’S DAY
SEHEMU YA SITA
susatule@gmail.com
SEHEMU YA SITA
susatule@gmail.com
Sikujua ni nini cha kufanya na wala sikujali hata yale maneno ya polisi ila nilichokuwa nikifikiria ni kwanini waliamua kuwaua Jamshid na Magret,,nilitamani kuona tena sura ya Jamshid pale nje lakini polisi walikataa kabisa nisimuone yeyote na hivyo sikufanikiwa kuiona maiti yake wala ya Magret,,hilo lilikuwa pigo kubwa katika maisha yangu,,nililia kwa uchungu sana hasa pale nilipofikishwa kituo cha polisi na kuandikishwa maelezo ya kuwa nimeua,,sikuweza kujibu chochote kwani sikuwa na la kujibu na ndipo hapo mkuu wa upelelezi wa kituo hicho alipowaamrisha askari wake niingizwe kwenye chumba maalumu cha mahojiano,,na huko hakuna rangi ambayo niliacha kuiona;
“tunataka utueleze kila kitu kwanini umefikia hatua ya kuua watu wawili na kujifanya kurudi ili usionekane kama umeua”,,haya yalikuwa maneno ya afande Magesa ambaye ni mkuu wa upelelezi kituoni hapo,,sikuwa na lolote la kujibu,,sikujua nimjibu nini,,sikuelewa ni kwa vipi nitaeleweka kwakuwa tayari ushahidi wa awali umeonyesha mimi ndiye niliyehusika kwenye mauaji,,,nilipigwa na nyaya za umeme na kuwekewa shoti ya umeme mpaka nilipopoteza fahamu na kuja kujikuta hospitali ya jeshi lugalo huku nikiwa na pingu mikono yangu yote miwili na pande zote nilizungukwa na maaskari,,kilio kilianza tena,,nilijutia situ kuzaliwa ila kila kitu katika maisha yangu kuligeuka na kuwa majuto kwangu.
****
“GEREZA LA UKONGA” ndilo jina la bango kubwa lililokuwa mbele yangu,,na hapo niligundua sikuwa tena mtu huru na sasa niliitwa mahabusu,,niliingizwa moja kwa moja mpaka mapokezi pale na hapo nilikutana mwanamke aliyejitambulisha kwangu kama afande Evelyn,,kwa sura tu alionekana kuwa mkorofi sana na hata kama ningeambiwa anavuta bangi wala nisingeshangaa,,,alinipiga kofi na kuniamuru nichuchumae chini,,nilimtazama usoni sikujua la kumfanya lakini hiyo haikuwa shida kwangu,,machozi yalikuwa yakiendelea kunitoka na kila mtu pale alidhani ya kuwa nilikuwa nikilia kwakuwa nilikuwa nikiogopa maisha ya gerezani lakini haikuwa hivyo nililia kwakuwa Jamshid na Magret watu pekee waliokuwapo kwenye maisha yangu hawapo tena na sasa sikuwa na mtu wa kumtegemea achilia mbali Gladys ambaye alikuwa ni rafiki lakini sikuwahi kumtilia maanani sio tu yeye hata Theresia…nilifanyia taratibu zote za pale magereza na kupelekwa mahabusu ambapo nilikaa chumba kimoja na Bibi Eunice Mkangala aliyekuwa na kesi ya mauaji ya mumewe,,afya yake ilikuwa mbaya sana na alikuwa amekonda mpaka anatisha,,Eunice alikuwa na miaka 50 na amekaa pale mahabusu kwa zaidi ya miaka mitano bila kesi yake kuisha na sasa alikuwa anakaribia kufa kwa kansa ya kizazi ambayo pamoja maombi ya muda mrefu kuomba kutibiwa hakuna yeyote aliyemsikiliza.
****
WIKI MBILI MBELE
Chakula kibovu na harufu mbaya ya chumba cha mahabusu ilikuwa imeshazoeleka ndani ya pua yangu,,machozi yalikuwa yamenitoka kwa muda wa wiki mbili nzima, na sasa yalikatika na kilichobaki ni majonzi ndani ya moyo wangu,,,asubuhi ilikuwa ni shwari na kajua kalianza kuonekana kupenya kwenye kadirisha kadogo kalikokuwa juu kabisa ya kile chumba. Sauti ya askari wa kike zilisikika kwa nje huku ikionekana kabisa walikuwa wakija chumbani kwenye seli yetu.
“ndiyo hapa fungua huku yule Malaya ndo kawekwa huku” nilisikia mmoja akimuelekeza mwenzake na kisha sauti za funguo zikifungua mlango mkubwa wa chuma zilisikika na sauti nyingine za wanaume zilisikika zikija upande uleule.
“afande fanyeni haraka ile gari kubwa itajaa,,hatuna gari ndogo leo zote zimeenda mkuza kwaiyo itabidi tumchanganye kwa wanaume kule” ilikuwa ni sauti ya askari wa kiume na hapo hofu ilianza kutanda tena lakini akili yangu ilirudi nyuma na kukumbuka kuwa nilitaarifiwa kuwa leo ndiyo ilikuwa siku ya mimi kupelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa aajili ya kusomewa mashtaka yangu kabla ya kesi yangu kuanzwa kusikilizwa katika mahakama kuu pale upelelezi utakapo kamilika.
“we muuaji sogea huku” ilikuwa sauti ya afande Evelyn ambaye sasa alikuwa ni kero nyingine kwenye maisha yangu,,,nilisogea karibu na mlangoni na kufanikiwa kuwaona maaskari magereza saba wa kiume waliokuwa wameshika bunduki,,macho yangu yalikuwa yamevimba kwa kulia lakini hakuna aliyeonekana kujali hilo.
“chukua hizi nguo vaa haraka” alinipa nguo zile na mimi nilirudi ndani kidogo ili niweze kuzivaa ila nilipewa kofi moja ambalo kama ningepewa nafasi ya kulielezea lile kofi limetoka kwa nani basi ningesema kwa shetani lakini haikuwa hivyo lilikuwa kofi toka kwa afande Evelyn lililofanya masikio yangu yazibe na damu kuanza kutoka puani,,sikuweza kunyanyuka pale chini na ndipo bibi Eunice huku akilia alikuja na kunisaidia kunyanyuka.
“nakupa nguo uvae unarudi ndani kuvalia huko ili nini wewe chokoraa,,,unajifanya unaogopa kuvua nguo mbele ya wanaume wakati we ni muuaji tu mbwa wewe,,vua hapa na uvae hizo” nilimsikia tena afande Evelyn akinifokea huku wale maaskari wa kiume wakimsifu kwa lile kofi,,haikuwa kitu kizuri kusifia lakini kila mmoja alionekana kufurahishwa na nilichofanyiwa,,nilivua zile nguo pale na kubaki uchi kama nilivyozaliwa na kisha nilianza kuvaa zile nguo nilizopewa pale huku damu ziliendelea kunitoka,,bibi Eunice alinisogelea na kutaka kunifuta lakini alipigwa teke lililomrudisha mpaka kwenye kona na chumba kile,,nililia kwa uchungu lakini nilikuwa najisumbua kwakuwa haikusaidia kitu kulia kwangu japo ilipunguza maumivu ndani ya moyo wangu,,wakati navaa zile nguo nilimsikia askari mmoja kijana akimueleza afande Evelyn kuwa amenipenda na wafanye kama kawaida,,sikujua maana ya maneno yao na wala sikuyajali,,nilifungwa pingu mikononi na nyororo miguuni kisha mlango ulifungwa na taratibu nilianza kusukumwa kuelekea nje,,nilipotoka pale niliandikishwa na hapo ndiyo maajabu mengine nilipoyaona,,niliingizwa kwenye gari lililokuwa na wanaume watupu ambao wengi walionekana kuwa ni majambazi sugu,,walipiga miluzi na kelele nilipoingizwa kwenye gari kisha gari lilianza safari ya kuelekea mahakamani,,nilifanikiwa kuona maeneo ya jiji na yalinifanya nijisikie uchungu sana,,sikujua kabisa nini itakuwa hatima ya maisha yangu japo nilitamani sana nife kuliko kuendelea kuishi mateso niliyokuwa nayapata toka kwa afande Evelyn yanifanya kabisa nisitamani kuishi hata dakika moja kila niliposikia akija kusogelea kile chumba kidogo nilichowekwa.
“MAHAKAMA YA HAKIMU MKAZI KISUTU” haya ndiyo maneno yaliyosomeka katika akili yangu na sasa tulikuwa tumefika, cha ajabu ni kundi kubwa la waandishi wa habari waliokusanyika pale nje wakisubiri taarifa yangu,,maaskari walinizuia kutoka na baada ya kushushwa wale wengine wote gari ile ilizungushwa nyuma ya mahakama ambapo hapakuwa na watu wengi na ndipo nilishuka na kupelekwa chumba cha kutunzia mahabusu kilichokuwa pale mahakamani,,nje ya chumba kile alikuwa amesimama jasusi afande Evelyn na maaskari wengine wa kikosi cha KMKM,,baada ya kama nusu saa nilisikia wakiongea kichinichini;
“huyu anaenda kwa nani” aliuliza askari mmoja wa kiume.
“faili lake limepelekwa kwa Mheshimiwa Mnyemi” alijibu askari mwingine na hapo maongezi mengine ambayo sikuyafurahia yaliendelea.
“sasa afande mimi huyu mahabusu nataka nirekebishe leo usiku maana nitakuwa lindo ila sasa siunajua bila wewe kunifungulia pale siwezi ingia kwakuwa kule wanaume haturuhusiwi” aliongea yule askari wa kiume.
“nyie vijana hamna ishu mwenzio afande Omary alikuwa anamfataga yule mama anayekaa na huyu toka enzi hizo akiwa na wiki moja pale mahabusu alivyomjinga akamtia na mimba,,mkanifanya nimehangaika kumtoa kinyemela ili mambo yasibume mpaka tumemsababishia mama wa watu kansa ya kizazi” alionge afande Evelyn.
“afande na wewe unawajali hawa Malaya wauaji tu,,hivi kwani yule maza alimuua nani”aliuliza yule askari na hapo ndipo nilipopata mda wa kujua kwanini bibi Eunice alikuwa pale mahabusu na mimi.
“yule mama alikuwa ananyanyaswa sana na mumewe alaf yeye ndiyo alikuwa kila kitu yani mume hohehahe tu lakini mume kwakuwa alijua kuwa mwanamke kwake haruki akawa analeta wanawake ndani kila siku, yule mama akawa anavumilia,jamaa akawa mara nyingine anampiga yule mama sana na kuna siku alimpiga mpaka mimba ikaharibika ila yule mama akawa anasamehe,,sasa kesi ilikuja kumpata siku moja amerudi toka kazini anafika ndani vitu vyote vimekombwa mumewe kahamishia kwa mwanamke mwingine,,sasa akapata taarifa kuwa vitu vyote na magari vimeamishiwa kwa huyo kimada si akaenda kule,,duuu! Akavikuta kweli akamuuliza mumewe akaanza kumpiga na kumwambia nani kamwambia aje pale,,alipokea kichapo bhana sasa yule kimada akanyanyua kisu amchome huyu mama sasa,,kile kisu nasikia kikamkosa kikamchoma huyo mwanaume na ndo kifo palepale,,kwaiyo yani huyu mama hakuua ila wale waendesha mashtaka walipewa ela za kutosha kesi ikamuangukia huyu aliyeenda kule” alihadithia afande Evelyn.
“du! Sasa na wewe ulijuaje?” aliuliza yule afande.
“mimi tena!hahaa,,,chezea mimi wewe..ulikuja mgao pale maana yule mzee alikuwa amekomba ela zote za mkewe akampa yule kimada,,kwaiyo ili kuziba watu mdomo kukatembea pesa chafu,,yule inspekta Rashid ikabidi anishirikishe kwakuwa yeye ndo alikuwa muendesha mashtaka,,nikakatiwa milioni zangu tatu nilipie wanangu ada maana kipindi icho ndo mwanangu kachaguliwa kwenda kidato cha kwanza alaf nilikuwaga na mkopo nikikatwa mshahara unabaki elfu ishirini,,ikabidi niile,,ila wengine naskia walipata mpaka milioni kumi,,na jaji yule alipigwa milioni 30,,na sasa hivi anavyoumwa hivi ndo wanasubiri tu afe basi” alihadithia kwasauti isiyokuwa na chembe ya aibu.
“du!ila dhambi sana afande” aliongea yule askari wa kiume.
“dhambi ndiyo ila ntafanyaje na mshahara haunitoshi,,wewe mtu nalipwa laki tatu na ishirini itatosha nini,,lazima wachache wateseke wengine waneemeke,,kwanza ela yenyewe imenipa gundu,,mototo mwenyewe akapata ziro kidato cha nne” aliongea huku akicheka.
“da!namuonea huruma sana” aliongea yule afande.
“unamuonea huruma huku unamtamani huyu,,yule mama alikuwa pande la mwanamke yani mzuri mpaka kila mtu anamtamani,,mi nikawa nakula tu ela kufungulia maafande waende wakatimize haja zao pale,,nilikuwa nakula hizi elfu kumi kumi hizi hadi raha”aliongea afande Evelyn lakini kabla hajamaliza alikatishwa na sauti ya karani wa mahakama iliyokuwa ikimuambia kuwa mahakama ilikuwa inataka kuanza.
Niliingizwa mahakamani na sasa nilikuwa na mawazo mapya juu ya aina ya maisha nitakayoishi huko mahabusu kwakuwa nilishapata picha ya nini kitatokea katika maisha yangu ya mahabusu,,,wakati napitishwa kwenye korido za mahakamani waandishi wa habari walikuwa wakihangaika kunipiga picha,,lakini mimi sikujali kitu,,nilikuwa nawaza juu ya maisha mapya ya kuuzwa na afande Evelyn,,niliwaza maisha ya kuitwa muuaji na huku si kweli kuwa nilikuwa muuaji,,nisingeweza kumuua Jamshid hata shetani anajua hilo,,haikuwa rahisi kumuua Magret kwakuwa yeye alimaanisha maisha kwangu,,yote yaliyosemwa na kuandikwa kwenye magazeti hayakuwa na ukweli wowote na wala hayakuukaribia hata ukweli halisi lakini sikuwa na namna ya kuuelezea ukweli zaidi ya pale mahakamani ambapo hata hivyo sikuwa na imani napo tena.
“kooooooootiiiiiiiiiiiii” ni sauti ya askari wa pale mahakamani iliyomaanisha kuwa sasa mahakama ilianza,,na watu wote walisimama,,bado machozi yaliendelea kunitoka na hakimu alinitazama kisha nilimsikia akiongea na upande wa mashtaka.
“vipi mko tayari kwa taratibu za awali au mmekuja kuomba adjournment (kuahirisha),,mana nimechoka na excuses (visingizio) zenu afande” aliongea hakimu aliyeonekana ni mtu makini.
“hapana mheshimiwa tupo tayari kwaajili ya kumsomea mashtaka yake na taratibu za upelelezi zinaelekea kukamilika mheshimiwa” aliongea askari mmoja wa jeshi la polisi ambaye kwa maelezo yake alikuwa ni mwendesha mashitaka na nilipomtazama niligundua ni yule aliyekuja pale kituoni siku hiyo nilipopelekwa,,alianza kusoma karatasi aliyokuwa ameishikilia pale mkononi na ambayo hata mimi nilipewa lakini sikuweza kuisoma kwakuwa nilikuwa nimejawa na machozi uso mzima, kwa mbali nilimsikia akiendelea kusoma ile karatasi.
“…ambapo anashitakiwa kwa kosa la mauaji ya Jamshid Jabir na Magret George kinyume na kifungu cha 196 cha kanuni za adhabu sura namba 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho yake mwaka 2002”..nililia sana ilipofika sehemu hii,,sikuwa nimeua kama wasemavyo lakini sikuwa namna ambavyo ningeeleza kuwa sio muuaji,,hakuna ambaye angeelewa kiukweli kuwa mimi sikuwa muuaji,,kila mtu alifikiri hivyo na pengine labda ushahidi ungenionyesha kuwa sijaua japo sikuelewa ni ushahidi wa aina gani ungetumika.
Baada ya kusomewa mashtaka yangu kesi yangu iliahirishwa mpaka mwezi mmoja mbele na dhamana yangu niliambiwa imefungwa kwakuwa kosa langu halina dhamana,,mpaka hapo sikuwa na wakili wa kunitetea lakini mahakama ilisemwa kutokana na ukubwa wa kosa langu serikali itaniwekea wakili wa kunitetea na mimi sikuwa na neno la kusema.
Safari ya kurudi ukonga ilianza na sasa mawazo yalinizidi kwa kuwa ni wazi sasa kuwa usiku wa leo yule askari angekuja kunibaka kama walivyokuwa wamekubaliana na afande Evelyn baada ya kumuahidi kuwa angempatia shilingi elfu 10.
“mbona wasichana wengi wanajiuza kwanini asingeenda kununua mapenzi mpaka anifate mimi,,ee mungu nisaidie” nilijisemea moyoni huku machozi yakinitoka,,hatimaye tulifika pale magereza na kuhesabiwa kama kawaida na maaskari walinisindikiza mpaka kwenye chumba changu ambapo nilimkuta bibi Eunice akiwa pale chini anatetemeka akidai kuwa anaumwa,,kabla wale maaskari hawajaondoka niliwasihi wampeleke hospitali kwani inaonekana teke alilopigwa asubuhi pale alipotaka kunifuta damu iliyokuwa ikinitoka puani lilimuumiza mapafu yake na sasa alikuwa akipumua kwa shida,,pamoja na kuomba sana hakuna aliyenisikia,,ndani ya kile chumba kulikuwa na mbu wengi na baridi kali iliyomfanya bibi Eunice azidi kutetemeka huku akipumua kwa shida,,sikuwa na jinsi ya kumsaidia zaidi ya kulia na kuzidi kumuombea lakini huo haukuwa msaada mkubwa,,nilivua nguo zangu zote na kumfunika yeye ili asipatwe na baridi na mimi nilijikunyata na kumkumbatia, hali hii ilinifanya niwakumbuke sana wazazi wangu hasa mama yangu aliyependa sana kunikumbatia kipindi nilipokuwa mdogo,,baridi la pale ndani lilikuwa ni kali na lilipenya hadi kwenye mfupa na kusababisha maumivu makali sana ya mifupa,,mawazo yalizidi kuniumiza zaidi pale nilipofikiria juu ya ujio wa yule askari kijana aliyemuambia afande Evelyn kuwa angekuja,,cha kushangaza nilipitiwa na usingizi lakini hakuwa aliyekuja.
***
Ilikuwa asubuhi tulivu nilishtuliwa na miale ya jua iliyochungulia katika dirisha letu pale chumbani,,niliamka na kukumbuka kuwa nilikuwa uchi kwakuwa nguo zangu nilimfunikia bibi Eunice ili kumkinga na baridi,,nilimuamsha lakini alionekana kuwa katika usingizi mzito na hivyo nilizichomoa zile nguo taratibu na kuzivaa,,baada ya hapo nilianza kumtikisa taratibu nikimuamsha ili tuweze kumuomba askari atakayekuja wampeleke hospitali,,nilijaribu kumuamsha kwa mda mrefu bila mafanikio na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa amefariki,,,nililia sana na kujiona kama mtu ninayesababisha vifo vya watu.
“afandee,,msaada tafadhali”,,nililia kwa sauti kubwa nikiomba msaada,,maaskari walikuja na kumshika mkononi na shingoni kisha waliangaliana wakimaanisha kuwa alikuwa amekufa tayari na kisha walimpigia simu afande Evelyn ambaye ndiye anayehusika na mahabusu na ndani ya dakika mbili alikuwa amefika pale na alipoambiwa kuwa bibi Eunice amefariki alinigeukia mimi;
“umemuua muuaji mwenzio si ndiyo?” aliniuliza na hapohapo kabla sijajibu alichukua kirungu na kuanza kunipiga mfululizo wakati wale wengine wakibeba mwili wa bibi Eunice,,sikujua kwanini huyu afande alinichukia hivi na wakati nilikuwa mwanamke mwenzake lakini nikakumbuka bibi Eunice aliwahi kuniambia kuwa Evelyn atanipiga ili nimuogope na ili siku akichukua fedha kwa maaskari wa kiume watakaotaka kuja kufanya mapenzi na mimi niwe na uwoga wa kuwakatalia au kumwambia mtu yeyote atakayekuja kunitembelea..alinipiga na kile kirungu kwa dakika kumi mfululizo na ndipo nilipopoteza fahamu,,nilikuja kushtuka kesho yake nikiwa hospitali,,nilifungua macho taratibu na kwa mbali niliweza kumuona askari aliyevaa koti jeupe na msichana mdogo aliyevaa suti nyeusi,,pembeni yangu kulikuwa na maaskari wadogo wakike,,walipoona nimeamka walimuita daktari ambaye alikuja mpaka pale na kuniambia nisijaribu kunyanyuka kisha alirudi tena kuongea na yule msichana na baada ya muda mfupi waliingia wote wawili ndipo nilipogundua kuwa alikuwa ni rafiki yangu Clara Mtei niliyesoma nae chuo kikuu Helnsik yeye akisomea shahada ya sheria, mimi na Clara tuliishi chumba kimoja chuoni wakati tunasoma lakini hakuwahi kuwa rafiki yangu mkubwa sana alikuwa ni rafiki wa kawaida tu ambaye hatukuwahi kujuana sana..nilipomuona nilihisi faraja imenijia moyoni mwangu,,nililia sana na Clara alishindwa kujizuia na alilia kwa uchungu mkubwa,,mara ya kwanza namuona Clara analia ilikuwa kwenye mahafali ambapo yeye ndiye aliyekuwa mwanafunzi bora wa kitivo cha sheria baada ya kupata shahada ya heshima ya daraja la kwanza(LLB Hons.) siku iyo Clara alilia lakini ilikuwa ni kilio cha furaha na sasa alikuwa analia kwa uchungu wa kunikuta katika hali kama ile;
“pole sana Faith” alinipa pole huku akilia
“asante Clara, why are you here”(kwanini uko hapa) kwa sauti ya kusuasua nilimuitikia na kumuuliza.
“I read from the newspaper, and I do believe u didn’t kill them”(nimesoma kwenye magazeti, na ninaamini hukuwaua) maneno haya ya Clara yalinipa moyo na sasa nilijiona yupo mtu anayeniamini.
“Yes I didn’t Clara,,how could I kill my lovely fiancée, how could I kill Magret”(ni kweli sikuua Clara, ningewezaje kumuua mchumba wangu kipenzi,,ningewezaje kumuua Magret),,kila mara nilipotaja jina la Jamshid au la Magret machozi yalinitoka.
“Am going to defend you,,am going to be your Lawyer Faith”(nitakutetea,nitakuwa mwanasheria wako Faith)
“Ooh asante sana Clara,,lakini najua lazima wataninyonga,,nimeambiwa adhabu yangu ni kunyongwa,,ila sijaua Clara, am not a murderer” (mimi si muuaji)
“Hata kama ungekuwa umeua usingenyongwa” aliniambia Clara huku akinitazama.
“kwanini” nilimuuliza kwa shauku
“KWASABABU UNA UJAUZITO WA MWEZI MMOJA” aliniambia Clara huku akitabasamu
“WHAAAAAAAAAAAAAT”
NINI KITAENDELEA??USHAHIDI UTAKUWAJE??JE CLARA ATAFANIKIWA KUMSAIDIA FAITH ATOKE??VIPI HARAKATI ZA AFANDE EVELYN ZITAISHIA WAPI??FREEMASON WATAMUACHIA FAITH?? KIFUNGU NAMBA 26 CHA KANUNI ZA ADHABU KINASEMA KAMA MWANAMKE NI MJAMZITO HATAHUKUMIWA KIFO BALI KIFUNGO CHA MAISHA,,,JE ITAKUWAAJEEE??
**FATILIA SEHEMU ZINAZOFATA**

No comments:
Post a Comment