SEHEMU YA NNE..THE WORST VALENTINE’S DAY

THE WORST VALENTINE’S DAY
SEHEMU YA NNE
susatule@gmail.com
ILIPOISHIA
,,,nilimtazama mama yangu aliyekuwa amekonda kupita
kiasi na ndipo nilipopaza sauti;
“COOOMEEEE THE ANGEEELLLLS OFFFF LIIIGGHHT”(njooni
malaika wa nuru),,,nilipaza sauti mara tatu na ngurumo kubwa za radi
ziliitikisa ile nyumba moto mkubwa ukawaka na mvua kubwa ikaanza kushuka,,,Jamshid
alinisogelea na lile panga kwa karibu na kuniuliza mimi ni nani na nina nguvu
gani,,,na mimi nilimjibu kwa sauti kuu…
“Am a FREEMASON”
SONGA NAYO
“unasema nini” nilisikia sauti ya Jamshid ikiuliza kwa
shauku ya kutaka kujua nilichokisema,,mda huo wale wengine wote waliyeyuka na
sikujua walitokaje pale,nilipotazama pale ndani hata hivyo nilimwona Magret tu
ambaye alikuwa bado pale chini.
“kama ulivyosikia”nilimjibu Jamshid na kukimbia pale
alipokuwa Magret nikamnyanyua na ghafla nilishangaa kuona lile ziwa likiwa
halijakatwa,,hapo bado ngurumo za radi na ule moto uliendelea kuwaka na ndipo
niliponyoosha ishara ya vidole viwili na pale kila kitu kilitulia,,,sikumwona
baba yangu wala mama yangu na pale ndani palikuwa shwari kabisa,,niligeuka tena
na sasa nilimuona Jamshiod aliyekuwa amesimama huku akitetemeka na mda huu
alikuwa katika hali ya kibinadamu..nilimsogelea na hapo nilipata ujasiri mkubwa
wa kumpiga kofi shavuni;
“nakuchukia kuliko kitu chochote katika maisha
yangu,,ondoka hapa”,,nilimwambia Jamshid na hapo nilishuhudia machozi yakimtoka
na sauti yake ilisikika ikiniambia;
“sina hatia,,ipo siku utaujua ukweli Faith” aliniambia
na muda huohuo sikumuoana tena,,nilikaa pale chini nikalia kwa uchungu sana na
ndipo nilipomwona Magret akifungua macho taratibu,,nilimkimbilia pale chini na
ndipo nilipogundua Magret hakufahamu lolote lililokuwa likiendelea;
“kwanini unalia dada Faith” ndilo swali la kwanza
alilonihoji na nilijitahidi kumficha ukweli wa mambo ili kama ni kweli
hatokumbuka basi katika maisha asikae akumbuke lile tukio lililotokea
pale,,sikutamani kabisa mtu yoyote afahamu kilichotokea kwakuwa hata mimi
nilitamani kuusahau ukweli niliouona,,,maswali mengi yalikijaza kichwa changu
lakini kikubwa ni wapi wamepelekwa wazazi wangu na ni kwanini Jamshid alibaki
nyuma,,mapenzi na Jamshid sikuyawaza tena na sasa nilihisi maisha yangu
yameshaharibika kabisa siri zangu zimeshabainika na sasa kila mtu atajua kuwa
najihusisha na kundi ambalo wengi wanaliogopa;
“dada Faith”,,ilikuwa sauti ya Magret ambaye alikuwa
tayari ameshaamka pale chini na nilimuona akiwa amesimama dirishani,,hapo woga
ukanijia tena upya.
“unasemaje”nilimuuliza kwa shauku maana alionekana na
yeye alikuwa akitazama nje.
“kuna magari matatu yameingia kwetu meusi,njoo uyaone”nilinyanyuka
pale nilipokuwa na moja kwa moja nilienda mpaka dirishani nakutazama nje, ndipo
nilipogundua kuwa walikuwa ni wakuu wa kundi la freemason nchini Tanzania,,hofu
ilinijaa na hapohapo nilisikia tumbo likikata,,nilimwambia Magret kuwa wale
walikuwa wageni wangu na nilimuomba aende chumbani,,,na mimi nilitoka taratibu
nikaingia chumbani nikavaa gauni langu refu na kisha nilitoka mpaka pale nje
ambapo moja kwa moja nilikutana na mzee Vladimir ambaye ndiye mwenye cheo
kikubwa kwa hapa Tanzania;
“vi salute nel nome di angeli della luce”(nakusalimu
katika jina la malaika wa nuru) nilimsalimu kwa lugha ya kiitaliano kwakuwa
ndiyo lugha niliyoambiwa kuitumia wakati nikisalimiana na mkubwa
wangu,,,alininyanyua pale nilipopiga magoti na kuniangalia machoni kisha kunipa
mkono kama tulivyozoea kupeana kwa ishara zetu,,,mawazo yangu yote hayakuwa
pale, nilikuwa nikiwaza ni nini kitatokea kwakuwa kwa mara ya kwanza sasa toka
nijiunge na kundi hili kwa ushawishi wa Mzee Rorbahcho aliyekuwa rafiki mkubwa
wa baba yangu mpaka leo hii sijawahi kufatwa na viongozi wangu na leo ikiwa ndo
nimetumia nguvu za wakuu wa nuru nimekuja kufatwa nyumbani,,hii kwangu ilikuwa
ni hofu nyingine tena,,,akili yangu ilivurugika na sasa nilianza kujuta kila
kilichotokea kwenye maisha yangu,,,saa yangu ya mkononi ilionyesha mda huo
ulikuwa ni saa 5 na dakika 33,,ikimaanisha siku ya wapendanao ilikuwa bado
haijaisha; nilipotazama vizuri alioongozana nao niligundua kuwa alikuwamo Mzee
Rorbahcho nae alikuja na kunishika mkono..mpaka hapo ile hofu ikaondoka na
ndipo niliposikia sauti ya yule kiongozi ikiniambia tena;
“Noi vi proteggera ma si fara presto il tuo
sacrifice”(tutakulinda ila utatoa sadaka yako muda sio mrefu)..milishtushwa na
neno sadaka lakini sikupata muda wa kuuliza kwani wale waliingia kwenye gari na
kuondoka,,,bado akili yangu ahaikuwa sawa na sasa nilikaa pale chini tena
nikilia,,,ila ghafla machozi yalinikauka baada ya kunyanyua uso wangu na
kumuona Jamshid akiwa amesimama mbele yangu na kunipatia kitambaa ili nijifute
machozi,,hasira zilinirudia tena na sasa nilitoka pale kwa kasi na kukimbilia
ndani nikachukua bastola yangu na kutoka nje ambapo nilimkuta Jamshid akiwa
amesimama palepale,,,niliikoki na kunyoosha kuelekea kwake na bila kuhoji mara
mbili niliifyatua risasa mara tano mfululizo lakini hakuna hata moja
iliyopenyeza mwili wake,,nilizidi kulia na kufyatua risasi ovyo huku
nikimulekea yeye lakini niliishiwa tena na machozi nilipoona na yeye alikuwa
akili,,katika hali isiyokuwa ya kawaida nilimtazama Jamshid na kumuonea huruma,,mara
hii na mimi machozi yalinitoka si kwasababu nyingine ila nahisi ni kwasababu ya
mapenzi niliyokuwa nayo kwa Jamshid,,nilijaribu kuidanganya nafsi yangu kuwa
namchukia Jamshid lakini haikuwa hivyo katika uhalisia wake,,nilimpenda Jamshid
kwa kila hali na kikuwa nilikuwa nikikumbuka aliponambia pale ndani kuwa
alikuwa kama mimi lakini alikuwa alivyo kwa makosa ya wazazi wake..nilimsogelea
pale alipokuwa amesimama na kwa sauti ya ukali iliyojaa mahaba nilimuuliza;
“unataka nini katika maisha yangu ewe jini usiye na
haya”nilijitahidi kumkazia macho ili asione udhaifu wa kihisia ulioanza kutanda
ndani ya uso wangu.
“Faith,,nililazimishwa kuwa hivi baada ya wazazi wangu
kukiuka masharti ya jini lililompa utajiri baba yangu,,,baba yangu alikuwa ni
mmiliki wa kisima kimoja cha mafuta huko uarabun,,kuna kipindi mafuta hayakuwa
yanapatikana kabisa na ndipo alipoamua kwenda kutafuta namna ya kuhakikisha
kisima chake kinatoa mafuta kama kawaida,,,alifanikiwa na kupewa kaya ya majini
ili kufanya usimamizi wa shughuli zake kwa ahadi kuwa angenitoa sadaka lakini
baadaye aliwakatalia na ndipo walipoanza kumuandama na kisha kumfilisi na
mwishowe walikuja kumuua na nililazimishwa kunywa damu yake na toka pale
niligeuka kuwa kama wao,,niliamia kisiwani nungwi chini kabisa ya bahari na
kuishi huko nikinywa damu za watu waliopotelea baharini kwa muda wa miaka 7 na
ndipo nilipopandishwa cheo na kuachiwa,,siipendi hali niliyopo na kwasasa
nimefukuzwa na hawataniacha mzima mpaka niende na wewe,,,naamini unaweza ni
saidia kwakuwa uwezo wako na wa watu wako ni mkubwa kuliko uwezo”,,,aliongea
hayo Jamshid huku machozi yakimtoka,,,nilisikia uchungu kwa yale machache
aliyoyaongea na hapo nilimfata na kumkumbatia,,,sikuamini kwa ulo msisimko
niliousikia wakati namkumbatia Jamshid pale nje,,nilimkumbatia kwa takribani
dakika tatu bila kumuachia na wala sikutamani kumuachia pia,,,alikuwa na mvuto
wa aina yake kwa hakika ya moyo wangu huyu ndo alikuwa chaguo langu.
****
Nilimvuta mpaka ndani na ndipo niliponyanyua simu yangu
ya mkononi nikampigia mzee Rorbahcho nikimuomba kuonana nae,,na yeye alinambia
tukutane mda ule ule,,Lapodiz café iliyokuwa mita mia tano toka pale
kwangu,,nilimuingiza Jamshid kwenye gari na kuondoa gari kwa kasi ya ajabu na
ndani ya dakika tatu tulishafika,,nilishukla na kumueleza mzee Rorbahcho kila
kitu na yeye aliniambia tunaweza kumsaidia Jamshid akarudi katika hali ya
kawaida kwakuwa katika ulimwengu wa nuru mengi yanawezekana,,,hapo tulipanda
gari yake na moja kwa moja tulielekea mpaka eneo letu la kukutania maarufu kama
MASONIC LODGE,,na pale aliniacha nje na yeye na Jamshid waliingia ndani ambapo
wakubwa wa kundi hili walikutana,,nilisubiri nje kwa masaa matatu na hapo
sikupata usingizi hata kidogo,,baadaye walitoka na sasa Jamshid alionekana ni
mzima kabisa,,nilielezwa kuwa watamlinda na hakuna nguvu inaweza kushindana
nao.
****
WIKI MBILI MBELE
Haikuwa rahisi kumuonyesha Jamshid hisia zangu tena kwa
siku zilizofuata japo aliishi nyumbani kwangu kwa takribani wiki mbili sasa mar
azote alikuwa akijitahidi kuomba msamaha na kunieleza yale yaliyotokea hayakuwa
katika mipango yake na sasa niliamua kumsamehe na sasa mapenzi yetu yalianza
upya,,,Jamshid alifanikiwa kuuingia mwili wangu na kuweka historia ya kuwa
mwanaume wa kwanza katika maisha yangu kushika mwili wangu na hata kuvua nguo
yangu ya ndani,,nilisikia maumivu makali siku ile lakini raha niliyoipata
iliziba maumivu yale niliyoyasikia,,na sasa maisha yalikuwa ni kati ya mimi na
yeye na Magret ndani ya jumba letu kubwa lililojitenga na maeneo ya watu wengine,,,bado
nilikuwa na hofu ya pengine labda hali ya hatari ingeweza kujitokeza tena
lakini kwa maisha niliyoyaanza na Jamshid niliamini ningekuwa salama
kabisa..nilimpenda Jamshid kuliko kitu kingine chochote,,upendo wangu kwa
Jamshid ulikuwa sawa na nilivyompenda Magret japo kwa Magret ulizidi kiasi
kwakuwa yeye alikuwa ni sehemu ya maisha yangu,,Jamshid na Magret kwasasa ndio
walikuwa baba yangu na mama yangu, niliwapenda sana na kila muda niliwafikiria
wao.
“pipiiiiii,,,,,pipiii” ilikuwa ni honi ya gari
iliyokuwa ikiashiria kuwa kuna gari nje lililotaka kuingia ndani,,nilichungulia
nje nikaona Juma ambaye ndiye milinzi mpya wa geti akiende kufungua geti
ilikuruhusu gari kuingia, nilibaki palepale dirishani kutazama ni nani
aliyekuwa akiingia na ndipo nilipogundua kuwa alikuwa mzee
Rorbahcho,,nilipomuona nilikumbuka siku ya kwanza mzee Rorbahcho alipokuja
kikazi nchini finland na kunichukua mpaka Uingereza, mzee huyu alikuwa kama
baba yangu kwakuwa kila nilipomuona alikuwa akinikumbusha juu ya baba yangu,,alikuwa
rafiki mkubwa sana wa kibiashara wa baba yangu hivyo mara nyingi nilimsikiliza
kwa yale aliyoniambia,,siku hiyo tulipoenda Uingereza alinielezea juu ya kundi
la freemasons,,ni yeye ndiye aliyenishawishi kuingia kwenye kundi hilo na baada
ya kunikutanisha na mzee Richardson White mkuu wa kundi hilo nchini Uingereza
basi nilikubali kwa moyo mmoja kujiunga na kundi hilo,,niliandikishwa kama
mwanachama wa kundi hilo nikiwa ndani ya SURREY PROVINCIAL GRAND LODGE iliyopo
kusini magharibi mwa Uingereza inayojumuisha maeneo ya Hampshire na Berkshire
na mengine,,yeye ndiye aliyenitolea kiingilio na kuhakikishwa nawekwa kwenye
Masoni lodge itakayoniwezesha kufanikisha kuhudhuria kila mkutano
utakaofanyika,,Surrey Lodge ilikuwa inawanachama zaidi ya mia 300 na Uingereza
yote katika Lodge zote zaidi ya 8000 ilikuwa inawanachama 300,000,,hivyo
kuingia kwangu ndani ya kundi la freemasons kulitengeneza upya sehemu ya maisha
yangu na uamini wangu,,nilidhani ningeiacha dini yangu lakini haikuwa hivyo
bali niliingia katika jumuiya kubwa iliyokuwa na msaada kwangu;
*****
Nilitoka nje baada ya kuhakikisha kuwa mzee Rorbahcho
alikuwa ndani ya geti langu na kwa haraka nilimfata pale alipokuwa na kusalimu
na yeye aliitika,,nilimkaribisha ndani lakini hakuingia badala yake alinipa
taarifa ambayo ilinifanya nilie na nianze kujuta tena;
“the angels of the light requires you to give your
sacrifice today night before 00:00”(malaika wa nuru wanataka utoe sadaka yak
oleo usiku kabla ya saa 6:00) aliniambia kwa sauti kavu isiyokuwa na mtikisiko
wala mawimbi.
“and what’s that sacrifice”(na ni sadaka gani)
nilimuuliza huku nikitetemeka,,nilitamani anijibu kuwa ilikuwa kiasi chochote
cha pesa lakini si anambie ilikuwa ni mtu tena.
“you choose between Jamshid or Magret”(utachagua kati ya
Jamshid au Magret),,
Daaaaah...isikose kusoma sehem zinazo fuata
kwa maon tuma sms tu
0718 363624
No comments:
Post a Comment