MBAKAJI
ERASTO MWAKYOMO (50) ANAYETUHUMIWA KWA UBAKAJI AKIWA KATIKA OFISI YA
MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE KABLA YA KUCHUKULIWA NA MWENYEKITI WA
DAWATI LA WATOTO NA UKATILI WA KIJINSIA MARY GUMBO.

MWENYEKITI WA MTAA WA MAPELELE CHRISTOPHER MWAKIBETE AKIANDIKA BARUA KWA WAZAZI NA MTUHUMIWA KUPELEKWA POLISI
BAADHI YA WAZAZI NA NDUGU WA WATOTO WAKIWA NYUMBANI KWA MWENYEKITI WA MTAA.
ERASTO
MWAKYOMA mwenye umri wa miaka hamsini mkazi wa mtaa wa Mapelele Kata ya
ILEMI jijini Mbeya anahojiwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za
kuwadhalilisha watoto wawili wa kike wote wakazi wa Mapelele.
Wazazi
wa watoto hao baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watoto hao ambao
mmoja ana umri wa miaka minne na mwingine mitano walitoa taarifa kwa
Balozi wa mtaa Bwana CASIAN MWEZIMPYA ambapo baada ya kutafakari kwa
kina aliamua kulipeleka suala hilo kwa Mwenyekiti wa Mtaa.
Mwenyekiti
wa mtaa Bwana CHRISTOPHER MWAKIBETE Aliamua kuwaita wazazi na mtuhumiwa
kuwahoji yaliyotukia ambapo nao watoto walipewa nafasi ya kueleza ambao
walieza kuwa ERASTO Alikuwa akiwashika sehemu za siri na kuwapaka
mafuta kabla ya kufanya nao mapenzi.
Baada
ya kusikiliza kwa makini MWAKIBETE aliamuru kuwa suala hilo ni la
kisheria na kitaalamu hivyo hawezi kuchukua hatua zozote bali suala
hilo analazimika kulipeleka Polisi ambapo Mwenyekiti wa Dawati la
watoto na jinsia MARY GUMBO Alimchukua mtuhumiwa hadi kituo cha Polisi
kati.
No comments:
Post a Comment