Saturday, October 26, 2013

Kombe la Dunia U20:Wasichana wa Tanzania wawatandika Msumbiji 10-0

 
Winga wa Tanzania, Theresa Yona akimtoka beki wa Msumbiji, Esperanca Malaita
Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
TIMU ya soka ya taifa ya wanawake kwa vijana chini ya umri wa miaka 20, The Tanzanites imeifunga Msumbiji mabao 10-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya Kwanza ya Kombe la Dunia kwa mabinti wa umri huo, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.

Katika mchezo huo uliohudhuria na mashabiki wachache mno, hadi mapumziko, tayari Tanzanites walikuwa mbele kwa mabao 5-0.

Bao la kwanza lilifungwa dakika ya sita na Neema Paul aliyeunganisha pasi ya Theresa Yona, kutoka wingi ya kushoto, wakati mfungaji bora wa michuano ya kimataifa ya Airtel Rising Stars iliyofanyika mwaka huu Nigeria, Shelder Boniface alifunga la pili dakika ya 24 baada ya kupangua ngome na kumpiga chenga hadi kipa.
Deonesia Daniel akafunga bao la tatu kwa shuti kali la mpira wa adhabu lililotinga moja kwa moja nyavuni dakika ya 32 na dakika ya 41, Amina Ali akafunga la nne kwa shuti kali kutoka nje ya eneo la mita 18.

Shelider Boniface alifunga bao ambalo lingekuwa la tano dakika ya 45, lakini refa Ines Niyonsara wa Burundi akakataa.
Kipindi cha pili The Tanzanites inayofundishwa na Rogasian Kaijage ilirudi na moto wake na kufanikiwa kupata bao tano, mfungaji Neema Paul aliyeunganisha krosi ya Theresa Yona.

Hatimaye Shelder alifunga bao la sita dakika ya 80 akimalizia mpira uliotemwa na kipa kufuatia shuti la Stumai Abdallah.

Dakika ya 82 Tanzania ikapata bao saba kupitia kwa Amina Ali aliyefumua shuti kutoka katikati ya Uwanja.
 
Mama yangu!! mchezaji wa TZ kapigwa kwanja.Kumbe na mabinti wanazijua hizi

 
Umeuona upaja wa Mtanzania ulivyo kamaa? huwezi amini ni msichana
 
Shelder Boniface alifunga bao tamu sana, akipiga chenga mabeki watatu na kipa wao
 
Kikosi cha Tanzania

No comments:

Post a Comment