Saturday, October 26, 2013

Picha 10 za kijana anayetumia kipaji chake kujipatia kipato ndani ya kivuko cha Magogoni(Kigamboni DSM)

Ni takribani mwaka mmoja toka kijana huyu aanze kuonekana akionesha sarakasi ndani ya Kivuko kwa nia ya kujipatia kipato. Mara nyingi huonekana sehemu ya juu ya kivuko cha Magogoni akiwafurahisha wasafiri huku akichombeza kwa mafumbo ambayo huashiria anahitaji kupewa hela ya kula.
Wakati akiendelea na onesho, watu humrushia fedha. Watu wengi hasa wageni wa Kigamboni huonekana kufurahishwa sana na onesho hili lisilo rasmi. Haijathibitishwa kama ameruhusiwa na uongozi wa eneo husika, kwani wafanya biashara ndogo ndogo hawaruhusiwi kufanya biashara eneo la hilo na ndani ya vivuko pia.
Hii staili anaiita 'marehemu kagoma kuzikwa'
Akijiandaa kufanya staili ya kunawa uso kwa mguu
Akinawa uso kwa mguu
Akijiandaa kufanya staili ya mtu mlemavu
Akisota kwa makalio kama mlemavu, kwa mujibu wake staili hiyo inaweza kutumika kuwadanganya watu wa usalama wadhani kuwa wwe ni mlemavu na kukuruhusu kuingia Uwanja wa Taifa bure kuangalia soka
Akiendelea kuonesha staili ya mlemavu
Akionesha uwezo wa kufanya 'push up'
Staili ya utembeaji wa mabaunsa (wanyanyua vitu vizito)
Staili ya utembeaji mabosi ambao wamesha jilimbikizia mali kwa ufisadi.Katunisha na kitambi cha kizushi
Hii inaitwa fainali uzeeni. Hapa anaonekana mzee aliyechoka baada ya kuuchezea ujana wake bila kijiwekea akiba.

No comments:

Post a Comment