Hivi ndivyo mtaa wa Congo Kariakoo DSM ulivyo furika leo kufuatia maandalizi ya sikukuu ya X-Mas. Ni kelele mtindo mmoja, kila mtu ananadi bidhaa yake. Inafikia wakati huelewi ni bidhaa gani inanadiwa, bali ni kelele tu. Maana kila mtu anapayuka kwa nguvu ili asikike kuzidi mwenzake.
Kama ilivyo ada wizi haukosekani eneo kama hili. Kila mara lazima usikie mtu akilalamika kuibiwa simu n.k. Hii ndiyo Congo, ukifika kuwa makini
No comments:
Post a Comment