Saturday, January 25, 2014

Akamatwa kwa kosa la kujifanya Koplo wa JWTZ



NewsImages/7096970.jpg
Mtuhumiwa pichani aliyevalia mavazi ya JWTZ akiwa katika kibano
Monday, January 20, 2014 11:32 PM
EDWIN John Mponji (31) anashikiliwa kwa tuhuma zakudaiwa kufanya uongo kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga kwa kujitambulisha kwamba yeye ni Koplo wa Jeshi la Wananchi [JWTZ].
Imedaiwa kijana huyo alifika katika ofisi hizo na kutaka kuonana na mkuu huyo na kujitambulisha kuwa ni askari kutoka jeshi hilo huku akiwa amevalia mavazi hayo hali ya kuwa yeye si askari kutoka jeshi hilo.

Imedaiwa koplo huyo feki alikuwa akihitaji kijana wake afanyiwe mpango wa kuingizwa katika Jeshi la Kujenga Taifa.

Mponji alikwenda katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Halima Dendego huku akijitambulisha kuwa yeye ni Ofisa wa JWTZ aliongozana na kijana Emmanuel Joseph akitaka afanyiwe mpango ili aweze apate nafasi.

Wakati wa maelezo yake ofisini hapo akatiliwa shaka na ndipo ikatolewa amri ya kushikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Ndipo ilipogundulika kuwa Mponji si askari kutoka JWTZ na alipopekuliwa zaidi nyumbani kwake alikutwa na sare za JWTZ zikiwa na cheo cha koplo.

Alipotakiwa kutoa maelezo ni wali alizipata sare hizo alishindwa kutoa majibu na katika mahojiano zaidi iligundulika baada ya kukiri kuwa aliwahi kumaliza mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa kikosi cha 841 KJ Mafinga.

Mkuu wa Wilaya hiyo alitoa agizo kutoka jeshi la polisi na jeshi la Wananchi mtuhumiwa huyo aendlee kubanwa ili mtandao wake ubainike

No comments:

Post a Comment