Saturday, January 25, 2014

Baba wa kambo awachoma moto watoto wawili huku mama yao akishangilia

Askari wanaharakati  wa dawati la mtandao wa jinsia kulia na kushoto wakiwa wamemkamata mama wa watoto  hao tayari kwenda polisi

Hapa wakiingia na mama huyo katika ofisi za dawati la jinsia mkoa wa Iringa


Hivi ndivyo watoto hao walivyougunzwa kinyama na baba wa kambo











Mrakibu mwandamizi wa polisi na mkuu wa dawati la jinsia na watoto mkoa wa Iringa ,Atupele Mwambunda akiwatazama watoto hao nje ya ofisi ya dawati la jinsia mkoa wa Iringa


Mama wa watoto hao Watende Sanga akiendelea kupika chakula baada ya watoto kuchukuliwa na polisi





Askari wa dawati la jinsia Iringa akiingia kumsimamia mama wa watoto hao kufunga duka lake kabla ya kuchukuliwa kwenda polisi





 Mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Iringa Atupele Mwambunda (kulia) akimhoji mama wa watoto hao Watende Sanga kuhusiana na ukatili uliofanywa dhidi ya watoto wake.


WAKATI wanaharakati mbali mbali wakiwemo wanaharakati wa mtandao wa kijinsia Tanzania (TGNP) ,wanaharakati wa haki za binadam,WAMA kuendelea kukemea na kuendelea kupinga vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia na uyanyasaji wa wanawake na watoto hata kulifanya jeshi la jeshi la polisi kuanzisha dawati maalum linaloshughulikia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ,baba wa kambo Mussa Mdetela aamua kuwatesa kinyama watoto wake kwa kuwachoma moto miguu wakituhumiwa kuiba Tsh 10,000


Wakizungumza kwa shida na mtandao huu watoto hao Baraka Rajab Mohamed anayesoma darasa la kwanza na Mood Rajab Mohamed anayesoma darasa la sita walisema kuwa ilikuwa ni siku ya tarehe 3 ambapo walichukua pesa hiyo kiasi cha Tsh 10,000 na kwenda kununua chakula baada ya mama yao kushindwa kuwaandalia chakula.


Hata hivyo Mood anayesoma darasa la sita msingi Lugalo alisema kuwa siku ya tukio mdogo wake alikwenda ndani na kuchukua kiasi hicho cha fedha na baada ya muda walishirikiana katika matumizi .
Watoto hao ambao wanadai kuwa baba yao mzazi Rajab Mohamed aliwaacha na sasa anaishi jijini Dar es Salaam na wao wamekuwa wakiishi na baba yao mdogo huyo ambae mara kwa mara amekuwa akiwaadhibu vikali.


Kwani walisema kuwa kutokana na mara kwa mara kushinda bila kula ndipo siku hiyo walipoamua kuchukua pesa hiyo ili kununua bagia na vitumbua ili kujikimu kwa njaa .
Hata hivyo walisema baada ya baba yao kurudi kutoka katika shughuli zake na kubaini kuwa fedha hiyo imechukuliwa ndipo alipowakamata na kuwafunga kamba na kuanza kuwatesa kwa kichapo ili waweze kusema mtu aliyechukua pesa hiyo.


“Alitufunga kamba miguuni na mikononi na kuanza kututesa kwa kutupiga na baada ya kuona hatusemi ndipo alipochukua makaratasi ya naironi na kutufunga miguuni kisha kuchukua kiberiti ,mafuta ya taa na kuwasha moto katika miguu yetu huku akiendelea kutupiga na moto ukiwaka miguuni….wakati huo mama alikuwa amekaa mlangoni akishangilia kuwa wapige sana mimi nimewachoka hawa watoto heri wafe tu” walisema watoto hao


Atupele Mwambunda mkuu wa dawati la jinsia mkoa wa Iringa ameuthibitishia mtandao huu juu ya tukio hilo na kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na kamwe hakitavumilika.


Alisema kuwa kuanzishwa kwa dawati hilo ni kutaka kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kama hivyo na kuwataka wazazi na jamii kuepuka kuchukua sheria mkononi kwa kuwatesa watoto kama hao ambao mwisho wa siku wanapoteza mwelekeo wa maisha.


Mwambunda alisema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kumkamata mama wa watoto hao Watende Sanga huku mzazi mwenzake Mussa Mdetele bado anatafutwa na jeshi la polisi ili kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatesa watoto hao.


Huku mama wa watoto hao akidai kuwa wakati baba yao mdogo akiwapiga watoto hao yeye hakujua kinachotokea japo alikuwa na taarifa ya kupotea kwa pesa katika duka na kuwa baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa ili kuwatibu kinyemela pamoja na kuwaombea ruhusa shuleni .


Pia mwanamke huyo aliomba kusamehewa kwa madai kuwa hakujua kama kushangilia wakati baba yao akiwatesa watoto hao ni kosa .

No comments:

Post a Comment