Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti. Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliyefika eneo hilo. |
Safari ya kuingia kwenye pori hilo kwenda kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo. |
Wakazi wa Mji wa Pongwe wakiuangalia mji huo kwa masikitiko makubwa. |
Huzuni ilitawala eneo hilo.
MTU
mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30 ambaye jina
lake halijafahamika mpaka sasa amekutwa akining'inia juu ya mti wa
Mwembe uliopo katika pori lililopo nje kidogo ya mji wa Pongwe, Mkoani
Tanga.
Hali
ya sintofahamu iliendelea kutanda katika eneo hilo huku kila aliyeweza
kufika katika eneo hilo la tukio akiwa na mshangao wa kipi kilichomsibu
mtu huyo mpaka kufikwa na mauti ya aina hiyo.
Mmoja
wa mashuhuda wa tukio hilo ambaye hakutaja jina lake,ameeleza kuwa
walipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja aliYekuwa
akichunga ng'ombe katika pori hilo ambaye jina lake halikuweza fahamika
mara moja,hali iliyowapekea kwenda moja kwa moja eneo la tukio
kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo,lakini kila aliyefika pale
hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda hutu huyo alikuwa ni
mgeni kijijini hapo.
Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo ili kuona kama ana taarifa zozote juu ya tukio hilo zinaendelea.
No comments:
Post a Comment