Mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya Habari viliripoti kuhusu mtu mmoja raia wa Sierra Leone, Abdul Koroma ambaye
alikuwa anashikiliwa na Jeshi la Magereza nchini kufariki dunia leo Dar
baada ya kupigwa risasi na askari Magereza wakati akijaribu kutoroka.
Mtu huyo alifikishwa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa mara ya kwanza mwaka 2013 kwa tuhuma za
kukutwa na dawa za kulevya na kushitakiwa.
Ameuawa katika uzio wa Mahakama
hiyo baada ya kumtoroka askari magereza aliyekuwa amemsindikiza
kujisaidia ambapo alijaribu kuruka ukuta wa mahakama hiyo.
Shuhuda mmoja wa tukio hilo amesema; “alikimbilia
kwenye ule ukuta pale, akapandisha mpaka pale juu… anataka arukie
upande wa pili magereza washatokea, wakaona hawawezi kukimbia yuko mbali
ndio wakampiga zile risasi kama tatu hivi ndio akafariki…”
Akizungumzia tukio hilo Msimamizi wa Mashtaka Mahakama ya Kisutu Tumaini Kweka amesema; “Wakati wapo kwenye sero ndipo yeye akajaribu kutoroka kwa kujaribu kuruka ule ukuta wetu wa Mahakama ndipo wanausalama wetu ambao wako hapa wakaweza kundhibiti…“
Kuwasikiliza shuhuda wa tukio hilo na msimamizi huyo wa mashtaka sauti iko hapa.
Mtuhumiwa wa madawa ya kulevya raia wa Sierra Leone akiwa amepigwa risasi baada ya kutaka kuwatoroka askari magereza katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment