MTWARA SI SHWARI WAKATI HUU.
MAPAMBANO kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Wananchi wa Mkoa wa Mtwara umefika katika hatua mbaya,kiasi cha mtu mmoja kudaiwa kujeruhiwa vibaya baada ya kurushiwa bomu wakati wa mashambulizi hayo katika eneo la Magomeni.
Mbali na kujeruhiwa kwa mtu huyo aliyekuwa katika maandamano ya kupinga Bajeti ya Wizar
a ya Nishati na Madini, Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pia imechomwa moto.
Taarifa zilizopo hivi punde zinadai kwamba wananchi wa Mkoa wa Mtwara wamefungiwa majumbani tangu asubuhi, huku
Jeshi la Polisi likifanya msako wa nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuwanasa watuhumiwa wanaodaiwa kuchochea maandamano hayo kwa njia ya vipeperushi.
Shuhuda wa wa tukio hilo ameeleza kuwa waandamanaji hao wameapa kufa endepo serikali itaendelea na mipango yake ya kusafirisha gesi hiyo hadi Jijini Dar es Salaam.
"Hali hapa ni mbaya, tangu asubuhi wananchi wote wamefungiwa ndani ya majumba yao, hakuna anayeruhusiwa kutoka nje,Polisi wanapiga mabomu ya machozi kila mtaa huku wakiwasaka watuhumiwa waliosambaza vipeperushi na kuwatawanya wandamanaji waliozagaa katika mitaa mbalimbali, mpaka hivi sasa kuna mtu mmoja ameripotiwa kujeruhiwa vibaya katika mashambulizi ya raia na Asakari Polisi wanaotumia mabomu ya machozi na silaha zigine za moto"alisema shuhuda wa tukio hilo.
Hata hivyo imedaiwa kuwa hali hiyo imesababisha barabara zote kufungwa kiasi cha kuzuia mabasi yanayoingia na kutoka katika mji huo toka asubuhi, kuna baadhi ya mitaa matairi yamechomwa moto barabarani, magari ya FFU yametanda kila kona za mji, huku taarifa zidi ikifafanua kwamba hakuna mawasiliano, milio ya mabomu inasikika kila kona na hali ya utulivu sio ya kuridhisha, Askari wa zima moto wamesambaa kuzima moto na kuna baadhi ya nyumba maeneno ya Shangani zimechoma moto.
No comments:
Post a Comment